Timu za JKT (wanawake na wanaume) ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo itakayomalizika Jumanne Aprili 26.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Mikono Tanzania (TAHA), David Kiami alisema maandalizi ya ligi hiyo yamekamilika na wanatarajia mwaka huu kutakuwa na ushindani mkubwa.
Kiami alizitaja timu za wanaume na wanawake zilizopata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya mwaka huu kutoka Bara JKT, Ngome na Magereza wakati Zanzibar itawakilishwa na JKU, Nyuki na KMKM.
Aliwataka wachezaji kuongeza juhudi kwa sababu uteuzi wa wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo huo watachaguliwa kupitia ligi hiyo.