Liverpool yatakata ugenini

07Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
LONDON, England
Nipashe
Liverpool yatakata ugenini

LIVERPOOL ikiwa na wachezaji 10 uwanjani, ilitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika mechi ya Ligi Kuu England.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Alex McCarthy na Christian Benteke aliyefunga kwa mkwaju wa penalti katika muda wa nyongeza baada ya kumaliza dakika 90.

Awali, kipa wa Liverpool, Simon Mignolet alifanya kazi ya ziada kuokoa hatari iliyoletwa langoni, Yannick Bolasie, kabla ya muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili Ledley kufunga bao la kwanza kwa Palace.

James Milner alitolewa nje baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano kwa mchezo mbaya dhidi ya Wilfried Zaha, lakini pamoja na upungufu wa wachezaji, Liverpool ilibaki mchezoni.

Makosa ya kipa McCarthy kushindwa kuondoa hatari mbali na lango lake, kulimpa nafasi Roberto Firmino kufunga bao la kusawazisha.

Alberto Moreno nusura afunge bao kwa Liverpool katika dakika ya 88 kama siyo shuti lake kushindwa kulenga lango.

Christian Benteke, aliyeingia akitoka benchi alifanyiwa madhambi na Damian Delaney na kuzaa penalti aliyoikwamisha mwenyewe wavuni na kuipa ushindi Liverpool.

Habari Kubwa