Lukaku, Werner nje mwezi mmoja

25Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Lukaku, Werner nje mwezi mmoja

WASHAMBULIAJI wa Chelsea, Romelu Lukaku na Timo Werner wanategemewa kuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki nne (mwezi mmoja).

Wachezaji hao waliumia wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Malmo, Jumatano iliyopita na klabu ya Chelsea imethibitisha kwamba, itawakosa kwa muda usiopungua mwezi mmoja.

Chelsea wanapitia ratiba ngumu kutokana na mashindano kuongezeka huku wakihitaji huduma za washambuliaji wao tegemeo ambao wameumia kwa pamoja.

Chelsea walianza kuwakosa wachezaji hao katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Norwich City uliopigwa Uwanja wa Stamford Bridge, Jumamosi wakati wakishinda mabao 7-0.

Pia nyota hao wanatarajia kukosa mchezo wa EFL dhidi ya Southampton kesho Jumanne na pia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle mwishoni mwa wiki.

Wachezaji wengine ambao ni majeruhi katika klabu hiyo ni Christian Pulisic na Hakim Ziyech ambao wamekosekana katika michezo mingi msimu huu.

Habari Kubwa