Makambo: Sikufuata Kiatu Ligi Kuu Yanga

24Sep 2018
Faustine Feliciane
DAR ES SALAAM
Nipashe
Makambo: Sikufuata Kiatu Ligi Kuu Yanga

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo, amesema anafikiria zaidi ubingwa kwa klabu yake na si tuzo binafsi.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo,

Akizungumza na gazeti hili juzi, Makambo, alisema anatamani kufunga katika kila mchezo ili kuisaidia timu yake kuweza kufanya vizuri katika ligi hiyo inayoendelea kwa sasa nchini.

"Kwangu ubingwa ndio kitu ninachokiwaza zaidi, najituma uwanjani ili kufikia malengo yangu ya kuisaidia Yanga kuchukua ubingwa, kama nitakuwa mfungaji bora hilo ni jambo la pili," alisema Makambo.

Makambo ambaye jana alitarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwenye mchezo dhidi ya Singida United, ameshaifungia timu yake mabao matatu.

Alisema ligi ya Tanzania inaonekana kuwa ngumu,  hivyo nahitaji kupambana.

"Ligi inaonekana kuwa ngumu... Huu ndio msimu wangu wa kwanza, lakini tayari nimeanza kupata dalili ya ugumu na upinzani wa ligi," alisema Makambo.

Yanga imefanikiwa kushinda michezo yake mitatu iliyocheza kabla ya mchezo wa Jana usiku dhidi ya Singida United.

Habari Kubwa