Makonda amkabidhi milioni 10 'baharia' Juma Kaseja

09Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Makonda amkabidhi milioni 10 'baharia' Juma Kaseja

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemkabidhi mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania Juma Kaseja kitita cha Shilingi Milioni 10 taslimu ikiwa ni sehemu ya motisha na zawadi ya kazi nzuri aliyoifanya jana wakati wa mchezo baina ya Tanzania na Burundi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

RC Makonda amemkabidhi Kaseja fedha hizo leo Septemba 9,2019 mbele ya Kocha wa Taifa Stars, Katibu Mkuu TFF na baadhi ya wachezaji waliomsindikiza.

Makonda amekipongeza kikosi kizima cha Timu ya Taifa Stars kwa kututoa kimasomaso kutinga hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2022.

Kwa upande wake Kaseja amemshukuru RC Makonda kwa kutimiza ahadi aliyoitoa ndani ya masaa machache baada ya mchezo huo kukamlika jana ambapo ameeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kitamsaidia katika mambo mbalimbali ya kusongesha gurudumu la maisha.

Jana Tanzania iliibuka na ushindi wa Penati 3 - 0 dhidi ya Timu ya Burundi baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo kwa kufungana 1-1 na kuongezewa dakika 30 bila timu yoyote kupata goli na kuingia kwenye matuta ambapo Mlinda mlango Juma Kaseja alifanikiwa kupangua mkwaju mmoja wa Penati.

Habari Kubwa