Manula ajipa matumaini Mbabane

15Mar 2017
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Manula ajipa matumaini Mbabane

GOLIKIPA namba moja wa Azam FC, Aishi Manula, amesema wataenda kushinda mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.

GOLIKIPA namba moja wa Azam FC, Aishi Manula.

Manula, ambaye juzi ameitwa kwa mara nyingine kwenye kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars', amesema anafahamu wana mtihani kwenye mchezo huo wa marudiano, lakini ushindi wa bao 1-0 walioupata wiki iliyopita utawapa faida.

"Hakika mchezo wa marudiano hautakuwa rahisi, lakini tunaenda kupambana kuanzia dakika ya kwanza mpaka mpira utakapomalizika," alisema Manula.

Aidha, alisema hawana haja ya kukata tamaa wakati wanaongoza kwa goli moja.

"Tuna uwezo wa kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano, tupo kwenye maandalizi na tuna uhakika wa kusonga mbele," aliongeza kusema Manula.

Kikosi hicho cha Azam kinahitaji ushindi wowote au sare ili kuweza kusonga mbele kwa hatua inayofuata ya michuano hiyo kufuatia ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza.

Habari Kubwa