Manula autaka Moto wa Mapinduzi Ligi Kuu

17Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Manula autaka Moto wa Mapinduzi Ligi Kuu

KIPA bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, Aishi Manula amesema anataka kuendeleza rekodi yake hiyo nzuri kinyang'anyiro cha ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

KIPA bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, Aishi Manula.

Azam FC itashuka dimbani kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kumenyana na Mbeya City kwenye mfululizo wa Ligi Kuu na Manula aliyedaka mechi tano za Kombe la Mapinduzi bila kufungwa hata bao moja, amepania kuendeleza rekodi hiyo.

“Ninajisikia faraja sana kuweza kutwaa tuzo hiyo, inaamanisha kuwa Azam tumerudi kwenye ubora wetu na kuonyesha kama sisi ni timu kubwa. Nataka rekodi yangu nzuri ya kutoruhusu bao Mapinduzi nirudi nayo kwenye Ligi Kuu pia,”alisema.

Pamoja na hayo, Manula amemshukuru Mungu kwa mafanikio hayo na kuomba amuwezeshe kufanya mengine makubwa.

“Ninaishukuru timu nzima kwa ujumla kwa kuweza kucheza vizuri hasa mabeki wameweza kunilinda vizuri na tumeweza kumaliza mashindano haya bila kuruhusu bao, pia ni kitu kizuri kwa sababu hili linakuwa kombe la pili kuchukua bila kuruhusu bao, kwanza Kagame tuliweza kulichukua bila kuruhusu bao na hili la Mapinduzi kwa hiyo ni kitu kizuri,” alisema.

Habari Kubwa