Marekani, Mexico, Canada wenyeji Kombe la Dunia 2026

14Jun 2018
Na Mwandishi Wetu
MOSCOW, Urusi
Nipashe
Marekani, Mexico, Canada wenyeji Kombe la Dunia 2026

FAINALI za Kombe la Dunia 2026, zitafanyika kwa pamoja Marekani Canada na Mexico, baada ya mataifa hayo kuipiku Morocco iliyokuwa nayo ikiwania kuandaa kinyang'anyiro hicho.

Mataifa hayo yameshinda kwa kura 134 zilizopigwa na wanachama wa Fifa huku Morocco ikiambulia kura 65 tu.

Fainali za Kombe la Dunia 2026, zitakuwa kubwa zaidi katika historia ya michuano hiyo, zikishirikisha timu 48 zitakazocheza jumla ya mechi 80 kwa zaidi ya siku 34.

"Soka ni mshindi pekee. Wote tunaungana katika soka," Rais wa Soka wa Marekani, Carlos Cordeiro alisema.

"Asanteni sana, kwa heshima hii ya kushangaza. Asanteni kwa kutupa nafasi hii ya kipekee."

Zote Mexico (1970 na 1986) na Marekani (1994) zimeshawahi kuandaa Kombe la Dunia, wakati Canada yenyewe iliandaa fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake mwaka 2015.

 

 

 

Habari Kubwa