Mashali, Mmarekani kuzikunja Julai 7

30Mar 2016
Dar
Nipashe
Mashali, Mmarekani kuzikunja Julai 7

BONDIA Thomas Mashali atazikunja dhidi ya bondia Godfrey Michael kutoka Marekani katika pambao la Julai 7 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

bondia, Thomas Mashali.

Pambano hilo linaloandaliwa chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBF) na litakuwa la raundi 12.

Akizungumza na gazeti hili jana, mratibu wa pambano hilo Kaike Siraju alisema maandalizi yako katika hatua za mwisho na wanaamini hiyo ni nafasi nyingine kwa Mashali kutangaza vyema jina la Tanzania.

Kaike alisema kampuni yake imejipanga kuendelea kuwatafutia mabondia nchini mapambano ya kimataifa kwa ajili ya kutimiza ndoto za kukuza mchezo huo na kurejesha heshima iliyowahi kupatikana miaka ya nyuma.

Hili litakuwa pambano la pili la kimataifa kwa Mashali baada ya kupoteza dhidi ya bondia kutoka Urusi mapema mwaka huu.

Habari Kubwa