Mayanga aita 23 Taifa Stars

09Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mayanga aita 23 Taifa Stars

KOCHA wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Salum Mayanga, amewaita wachezaji 23 kujiandaa na michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya  Kongo na Algeria.

KOCHA wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Salum Mayanga.

Kikosi hicho kitaingia kambini Machi 18 jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria utakaochezwa ugenini Machi 22.

Mara baada ya mchezo huo, Stars itarejea Dar es Salaam kuumana na Kongo machi 27 kwenye uwanja wa Taifa.

Wachezaji walioitwa na timu zao kwenye mabano ni pamoja na magolikipa, Aishi Manula  (Simba), Ramadhani Kabwili  (Yanga) na Abdulrahman Mohamed (JKU) Mabeki ni pamoja na Shomari Kapombe, Erasto Nyoni (Simba), Hasan Kesy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani (Yanga) pamoja na Abdi Banda wa Baroka ya Afrika Kusini.

Viungo ni pamoja na Hamisi Abdallah  (AFC Leopards ya Kenya), Mudathir Yahaya (Singida United), Said Ndemla,  Shiza Kichuya (Simba), Faisal Salum (JKU), Abdulazizi Makame (Taifa Jang’ombe), Farid Mussa ( Teneriffe ya Hispania), Thomas Ulimwengu  (FK Sloboda Tuzla), Ibrahim Ajib  (Yanga) pamoja na Mohamed Issa  (Mtibwa)Kwenye kikosi hicho washambuliaji ni pamoja na Mbwana Samatta (Genk ya Ubelgiji), Saimon Msuva (El Jadida ya Morocco), John Bocco (Simba) na  Zayd Yahaya (Azam).