Mayanga aiwaza tano bora Bara

16Mar 2016
Dar
Nipashe
Mayanga aiwaza tano bora Bara

LICHA ya timu yake kupoteza mchezo dhidi ya Simba, kocha mkuu wa Tanzania Prisons, Salum Mayanga, amesema bado anaamini kikosi chake kitamaliza ndani ya nafasi tano za juu za Ligi Kuu Bara msimu huu.

kocha mkuu wa Tanzania Prisons, Salum Mayanga

Mayanga aliiambia Nipashe jana kuwa bado wana nafasi ya kupambana katika mechi nyingine zilizosalia kwenye ligi na kufungwa na Simba siyo mwisho wa ligi hiyo.

"Siwezi kuwalaumu sana wachezaji wangu, isipokuwa nitakwenda kufanya marekebisho madogo yaliyojitokeza ili kuhakikisha timu haishuki na inamaliza kwenye tano bora msimu huu," alisema Mayanga.

Alisema kikosi chake kimerejea jijini Mbeya kujiandaa kwa mchezo unaofuata dhidi ya African Sports utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jumamosi.

Prisons kwa sasa inakamata nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na mtaji wa pointi 36 baada ya mechi 23.

Habari Kubwa