Mayanja naye amlilia Dhaira

30Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mayanja naye amlilia Dhaira

KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja amesema kifo cha aliyekuwa kipa wa timu hiyo na timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes), Abel Dhaira (28) kimemsikitisha.

kocha wa simba jackson mayanja.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni juzi, Mayanja alisema Dhaira alikuwa ni kipa mwenye kipaji na katika kudhihirisha hilo, akiwa na miaka 23 aliweza kuiongoza The Cranes kutwaa mataji mawili ya Chalenji.

"Ameondoka mapema, hasa kwa nafasi yake, huu ndiyo ulikuwa muda muafaka kulitumikia taifa lake na klabu," alisema Mayanja ambaye ni Mganda pia.

Dhaira aliyekuwa akicheza IBV Vestmanaeyjar ya Iceland alikuwa langoni wakati Simba ilipotoka sare ya mabao 3-3.
Mapema Januari mwaka huu, Dhaira aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa kansa ya utumbo akiwa Ice Land.

Kabla ya kujiunga na Simba, Dhaira aliwahi kuzichezea klabu za Express na URA za Uganda na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Habari Kubwa