Mayay aeleza kilichofanya jina lake kukatwa urais TFF

17Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mayay aeleza kilichofanya jina lake kukatwa urais TFF

ALIYEKUWA mgombea wa urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mayay, amekiri kustahili kukatwa katika kinyang’anyiro cha kugombea wadhifa huo kutokana na kutofikisha idadi ya wadhamini wadhamini aliotakiwa kuwa nao ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini watano.

Ally Mayay.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mayay ameeleza kuwa aliwasilisha vitu vyote vinavyotakiwa ikiwamo vyeti lakini upande wa wadhamini hawakukamilika.

“Kati ya vitu vilivyotakiwa kuwasilishwa kama vile kitambulisho cha uraia, vyeti vya shule na barua za wadhamini watano, lakini mimi nimepata mdhamini mmoja,” Mayay.

Amesema kuwa amejitahidi kuomba udhamini katika klabu zote 18 za Ligi Kuu Tanzania Bara lakini mmoja ndiye alimuunga mkono.

“Nitaendelea kutoa mchango katika soka kwa nafasi nilikuwa nayo, pia nipo tayari kutoa ushauri kwa wagombea wakihitaji sera zangu nilizotakiwa kuwasilisha kipindi cha kampeni,” Mayay

Habari Kubwa