Mbappe azungumzia penalti ya Messi

09Dec 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mbappe azungumzia penalti ya Messi

KYLIAN Mbappe amesema Paris Saint-Germain itakwenda "kumhitaji Lionel Messi" wakati Mfaransa huyo akibainisha kwanini aliacha nafasi ya kufunga ‘hat-trick’ kwa penalti katika ushindi mabao 4-1 dhidi ya Club Brugge.

Mbappe alifunga mara mbili ndani ya dakika saba za mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kabla ya kumtengenezea bao Messi.

Licha ya kuwa na nafasi ya kufunga hat-trick, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hakuchukua jukumu la kupiga penalti iliyopewa PSG kipindi cha pili, na kumwachia, Messi afunge bao lake la pili kwenye mchezo huo.

Mbappe alielezea hiyo ilikuwa ni muhimu zaidi kwa Messi, ambaye maisha yake ya soka nchini Ufaransa bado hajakuwa na mafanikio makubwa sana wakati akiendelea kuzoea mazingira.

"Tunakwenda kumhitaji Lionel Messi," alisema Mbappe baada ya mchezo huo akiwaambia waandishi wa habari.

"Anabakia kuwa Lionel Messi. Tunakwenda kumhitaji wakati wa msimu, na nina uhakika atatusaidia kwenye mechi muhimu sana.

"Anatakiwa kujiamini kwenye mechi hizi. Ni nzuri kwa upande wake kumaliza mchezo akifunga mabao mawili, lakini ni nzuri kwa upande wetu na kwa baadaye."

Habari Kubwa