Mbaya wa Yanga atwaa tuzo

12Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mbaya wa Yanga atwaa tuzo

MSHAMBULIAJI wa Mbao FC, Habib Kiyombo , amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi kuu wa mwezi Desemba.

MSHAMBULIAJI wa Mbao FC, Habib Kiyombo.

Kiyombo ambaye katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu kabla haijasimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, aliifunga Yanga mabao mawili na kuipa ushindi timu yake ya bao 2-0 dhidi ya mabingwa hao watetezi.

Kiyombo, alifunga mabao hayo kwenye mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Desemba 31.

Kiyombo, aliwashinda wachezaji wenzake wawili waliongia fainali kuwania tuzo hiyo ya kila mwezi ambapo mshindi anapewa fedha Shilingi milioni moja.

Mabao mawili aliyoyafunga kwenye mchezo dhidi ya Yanga, yamemfanya Kiyombo kufikisha mabao saba mpaka kufika sasa kwenye ligi kuu.

Kiyombo amezidiwa bao moja tu na kinara wa mabao, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.

 

Habari Kubwa