Mbeya City, Ndanda zaweka rekodi

11Feb 2016
Adam Fungamwango
Dar es Salaam
Nipashe
Mbeya City, Ndanda zaweka rekodi

HATIMAYE timu ya Mbeya City na Ndanda FC zimeshinda mechi zao kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/16 zikiwa ugenini.

NDANDA FC

Timu hizo hazikushinda mechi yoyoye ugenini hadi ilipofika raundi ya 17 ndipo zilizopofanya hivyo. Mbeya City ilishinda mechi yake ya kwanza ugenini kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam Februari 4, ilipoifunga JKT Ruvu mabao 2-1 yaliyofungwa na Hassan Mwasapili na Yohana Morris, huku la kufutia machozi wa JKT likifungwa na Mussa Kimbu.

Siku hiyohiyo, Ndanda FC ilishinda mechi ya kwanza Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga kwa kuifunga Coastal Union bao 1-0. Bao pekee lilifungwa na Brayson Rafael anayeichezea timu hiyo kwa mkopo akitokea Azam FC.

Hadi sasa Mbeya City imecheza mechi 18, ikiwa na pointi 18 wastani wa pointi moja kila mchezo, ikikamata nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ikishinda mechi nne, sare sita na kupoteza mechi nane.

Ndanda inashika nafasi ya 10, ikiwa na pointi 17 kwa kushinda mechi tatu, sare nane na kufungwa mechi saba hadi kufikia raundi ya 18 ya Ligi Kuu.

Habari Kubwa