Wawili hao walikutwa na kosa la kushinikiza kuiondoa timu dakika ya 23 kinyume na kanuni ambayo iliainisha walipaswa kusubiri kwa dakika 30 na endapo gari la wagonjwa lisingewasili ndipo wangekuwa na haki ya kutoshiriki mchezo dhidi ya Namungo.
Mbwana Makata, David Naftar waiomba radhi TFF
22May 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Mbwana Makata, David Naftar waiomba radhi TFF
KOCHA Mkuu na Meneja wa Klabu ya Mbeya Kwanza, Mbwana Makata na David Naftar wameliomba radhi Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi kwa tukio walilolifanya na kusababisha kufungiwa kwa miaka mitano kutojihusisha na soka.
