Mgosi adai haumii kuketi benchi

06Apr 2016
Somoe Ng'itu
Dar
Nipashe
Mgosi adai haumii kuketi benchi

NAHODHA wa Simba, Mussa Hassan 'Mgosi' amesema haumizwi kukaa benchi kwenye Ligi Kuu Bara.

Mussa Hassan 'Mgosi'.

Mgosi alirejea Simba msimu huu akiwa ni mchezaji huru kutoka Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani, Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mgosi alisema kukaa kwake benchi ni uamuzi wa kocha.

Mgosi aliongeza siku zote amekuwa akiheshimu uamuzi wa benchi la ufundi.

"Ninaheshimu uamuzi wa kocha, wachezaji tuliosajiliwa ni lazima tukubali kile anachoamini kocha," alisema na kuongeza:
"Kila mtu hupangwa kulingana na aina ya mpinzani na nafasi yako kwa wakati huo."

Mgosi hajafunga bao tangu kuanza msimu huu na muda mwingi amekuwa akimsaidia kusimamia mazoezi Kocha Jackson Mayanja.

Habari Kubwa