Migi: Yanga hawatoki kwa APR

09Mar 2016
Lasteck Alfred
Dar
Lete Raha
Migi: Yanga hawatoki kwa APR

KIUNGO wa Azam, Mnyarwanda Jean - Baptist Mugiraneza ‘Migi’ amesema kuwa haoni jinsi Yanga watakavyoweza kuifunga timu ya APR kwenye mchezo wa hatua ya awali ya klabu Bingwa Afrika.

Jean - Baptist Mugiraneza ‘Migi"

Kiungo huyo wa zamani wa Kiyovu SC na APR (zote za Rwanda) alisema, “Yanga itapata ugumu kuifunga APR kama wataenda kwa akili ya kucheza mpira wenye utulivu. Wanachotakiwa kukifanya ni kucheza nguvu ili waweze kuvuruga mipango ya wachezaji wa APR.

“ Nimecheza APR kwa miaka tisa, ninafahamu vyema soka lao. Wanacheza kwa ubunifu zaidi kuliko nguvu. Kama unataka kuwashinda basi usikubali kucheza kama wanavyocheza wao. Huwa ni wajanja na wanaopenda kucheza mpira wa pasi nyingi na mashambulizi ya kushtukiza.

“ Ikitokea Yanga wakashindwa kuvuni mbinu bora za kuwakabili, huenda wakafungwa mabao mengi kutokana na jinsi timu hiyo imekuwa ikijiandaa mara kwa mara inapokuwa inakabiliwa na michezo ya kimataifa,”alieleza.

Kiungo huyo pia alieleza kuwa ubora wa APR upo zaidi kwenye safu ya kiungo. “Wana viungo hodari na wabunifu. Wengi wao wanafanana kiuchezaji na kiungo Haruna niyonzima.”

Habari Kubwa