Mingange alaani rafu aliyochezewa Msuva

03Apr 2016
Lete Raha
Mingange alaani rafu aliyochezewa Msuva

KOCHA wa timu ya soka ya Ndanda FC Meja mstaafu Abdul Mingange amesema nidhamu ni suala kubwa linalochangia timu yake kupata matokeo mabovu uwanjani.

KOCHA wa Ndanda FC Meja mstaafu Abdul Mingange

Kauli ya Mingange imekuja baada ya mchezaji wake Paul Ngalema kumchezea rafu mbaya Simon Msuva wakati akijiandaa kwenda kufunga bao katika michuano ya kufuzu robo fainali ya mashindano hayo.

Akizungumza alisema haikuwa na haja ya kukwamtua Msuva ndani ya 18 angemwacha wenda Kipa wake angeweza kuokoa bao.

Alisema lakini ukosefu wa nidhamu uwanjani kwa baadhi ya wachezaji wake kumechangia kupoteza mchezo huo.
Alisema kikosi chake kimecheza vizuri na kuweza kupeleka mashambulizi langoni mwa Yanga na kufanikiwa mabao mawili ambapo moja likakataliwa kutokana na mwamuzi kudai mchezaji kaotea.

Alisema baada ya matokeo hayo,kikosi kinaelekeza nguvu katika mchezo wao dhidi ya Prisons ya Mbeya wa Ligi kuu ya Bara.

Alisema atakifanyia marekebisho machache ili kiweze kupata pointi tatu muhimu katika mchezo huo.

Akizungumzia mchezo huo kwa ujumla, alisema utakuwa mgumu, kutokana na kwamba timu zote zitacheza kwa ushindani ili kuhakikisha wanatwaa pointi tatu katika mechi hiyo. Alisema timu yake iko Mtwara ikiendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo.

Habari Kubwa