Miraji anukia Kiatu Mapinduzi Cup

13Jan 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Miraji anukia Kiatu Mapinduzi Cup

WAKATI michuano ya Kombe la Mapinduzi ikimalizika leo kwa Simba na Yanga kucheza fainali, straika wa 'Wekundu wa Msimbazi' hao, Miraji Athuman, ndiye anayeongoza katika mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu cha mashindano hayo.

Simba ambayo imetinga fainali kwa kuitoa Namungo FC kwenye mechi ya nusu fainali iliyopigwa juzi katika Uwanja wa Amaan, inakutana na Yanga leo ambayo nayo juzi iliitoa Azam FC kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Hadi sasa kabla ya mechi ya leo, Miraji amecheka na nyavu mara nne kwenye michuano hiyo iliyoshirikisha timu tisa zikiwa katika makundi matatu mwaka huu huku Simba ikiwa Kundi B sambamba na Chipukizi ya Pemba na bingwa mtetezi, Mtibwa Sugar.

Miraji alianza kucheka na nyavu dhidi ya Chipukizi, akifunga mabao mawili Simba ikishinda 3-1 na kisha kutupia moja wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kabla ya juzi kuziona nyavu tena wakishinda 2-1 dhidi ya Namungo FC.

Mchezaji anayemfuata kwa karibu katika mbio hizo za kuwania ufungaji bora wa Kombe la Mapinduzi ni mshambuliaji mwenza wa Simba, Meddie Kagere pamoja na Steven Sey wa Namungo FC ambao kila mmoja amezifumania nyavu mara mbili...soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

 

Habari Kubwa