Mkenya atoa darasa la mbio nchini

14Feb 2016
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Mkenya atoa darasa la mbio nchini

MWANARIADHA wa mbio ndefu kutoka nchini Kenya,Teglalo Roupe amewataka wanamichezo nchini kucheza kwa kujituma ili wapate mafanikio.

Roupe alisema hayo wakati wa Semina ya kamisheni ya wachezaji iliofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi, Kibaha mkoani Pwani.

Roupe alisema mchezaji wa mchezo wowote anapaswa kucheza kwa bidii ili kupata mafanikio yatakayowasaidia mara baada ya kustaafu kucheza.

"Msikubali kutumika bila sababu ya msingi. Wanariadha tumikeni pale kwenye sababu za msingi kama mashindano makubwa yanayojulikana," alisema mwanariadha huyo.

Naye Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid alisema wachezaji wanatakiwa kujiwekea malengo ya kusoma na kucheza ili kujiongezea ujuzi utakaowasaidia baada ya kustaafu.

Pia aliwataka kuwa na malengo wakati bado wana uwezo wa kucheza na kushiriki mashindano mbalimbali.

Katibu wa TOC, Fribert Bayi alisema katika semina hiyo iliyoendeshwa na mkufunzi kutoka Ufaransa, Tounkara Kady Kanoute, wanamichezo 29 walishiriki.

Habari Kubwa