Mkutano Mkuu TFF wasogezwa mbele

07Dec 2018
Renatha Msungu
Dar es Salaam
Nipashe
Mkutano Mkuu TFF wasogezwa mbele

MKUTANO Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliokuwa unatarajiwa kufanyika Desemba 29-30 mwaka huu huko Arusha, sasa umesogezwa mbele hadi Februari 2 mwakani, imefahamishwa.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, picha na mtandao

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema kuwa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana jijini Dar es Salaam Novemba 29 mwaka huu, ndio kimesogeza mkutano huo ili kukidhi matakwa ya katiba ya shirikisho hilo.

Ndimbo alitaja sababu iliyosababisha kusogeza mkutano huo ni kuendana na kalenda ya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizowazi uliotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo mapema wiki hii.

Alisema kuwa uchaguzi huo mdogo utahusisha nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayewakilisha Lindi na Mtwara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayewakilisha Simiyu na Shinyanga.

"Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu lilianza Desemba 4 mwaka huu na mwisho utakuwa Desemba 9, 2018. Fomu zinapatikana kwenye makao makuu ya TFF na katika shirikisho," alisema Ndimbo.

Mbasha Matutu (Simiyu na Shinyanga) na Dustan Mkundi, walifungiwa maisha kujishughulisha na soka maisha kutokana na kukutwa na makosa ya udanganyifu.

Habari Kubwa