Mohamed Samatta njiani Ulaya

07Feb 2016
Lete Raha
Mohamed Samatta njiani Ulaya

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya soka ya Mgambo JKT, Mohamed Samatta, amesema mipango yake ya kucheza soka la kulipwa nje ya Afrika bado ipo, lakini kinachosubiriwa ni muda tu.

Kiungo huyo ambaye ni kaka wa mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars‘, Mbwana Samatta, ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji, alisema atafuata nyayo ya mdogo wake kucheza soka nje ya nchi kwa kuwa soka ndiyo kazi yake.
“Bado siwezi kuweka wazi kila kitu kwa kuwa mipangilio haijawa sawa, lakini mambo yakiwa poa kila kitu kitakuwa hadharani,” alisema Samatta.
Akizungumzia kuhusu ndugu yake anayekipiga katika klabu ya Genk FC ya Ubelgiji, alisema nidhamu, kujituma na kufuata maelekezo ya mwalimu ndiyo kilichomsaidia, hivyo naye atafanya hivyo ili kufika alipo Mbwana.
“Huwezi kutenganisha mpira wa miguu na nidhamu, ukitaka kuwa mchezaji mzuri lazima uhakikishe unafuata maelekezo ya mwalimu,” alisema.

Habari Kubwa