Morocco atoa sababu Simba kuitoa Namungo

13Jan 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Morocco atoa sababu Simba kuitoa Namungo

BAADA ya kufurushwa nje na timu ya Simba katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi juzi,Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hemed Morocco, amesema makosa madogo waliyoyafanya pamoja na kucheza mechi mfululizo katika mashindano hayo ni miongoni mwa sababu zilizochangia kutolewa.

Aidha, Morocco alisema hii ni mara ya kwanza kwa Namungo kushiriki Kombe la Mapinduzi, hivyo kukosa uzoefu wa michuano hiyo pia ni sababu nyingine ya kutolewa na Simba baada ya juzi kukubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amaan.

"Kama mwalimu sikufurahia matokeo hayo, lakini nawapongeza wachezaji kwa kujituma na kufanya vizuri pale walipopata nafasi za kufunga na hata kuokoa ila haikuwa bahati kwao.

"Wachezaji wamejituma, wameonyesha uwezo wa kufanya vizuri katika michezo yote tuliyocheza, naamini tutafanya vizuri zaidi katika michuano mingine na ijayo iwapo tutapata nafasi ya kushiriki," alisema.

Akizungumzia suala la waamuzi waliochezesha mchezo baada ya wachezaji wake kuonekana wakiwalalamikia mara kwa mara hususan mwamuzi wa kati, Mohamed Kassim, Morocco alisema walichezesha vizuri ila malalamiko hayo yalichangiwa na ugumu wa mchezo huo na kama kuna upungufu kidogo ni makosa ya kibinadamu ambayo ni kawaida kutokea mchezoni....soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa