Morrison awaita mashabiki Taifa

10Jul 2020
Faustine Feliciane
Dar es Salaam
Nipashe
Morrison awaita mashabiki Taifa

BAADA ya kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi walioupata dhidi ya Kagera Sugar juzi, kiungo mwenye 'mbwembwe' wa klabu ya Yanga, Bernard Morrison amesema hizo ni salamu kwa wapinzani wao kwenye mchezo wa Jumapili wa hatua ya nusu fainali ya kombe la FA na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kuji

Yanga Jumapili itawakabili Simba kwenye hatua hiyo ya nusu fainali, mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa timu hizo mbili.

Morrison, alisema kuwa goli alilolifunga linampa mzuka wa kufanya vizuri kwenye mchezo unaofuata na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ya FA.

Alisema mashabiki hawana haja ya kuwa na hofu na mchezo huo kwa kuwa yeye na wachezaji wenzake wanatambua umuhimu wa mchezo huo. "Lengo ni kufanya vyema na kuhakikisha tunacheza fainali ya FA, tunafahamu ndio tiketi yetu ya pekee kucheza mashindano ya kimataifa," alisema Morrison na kuongeza,

"Muda uliobakia naamini benchi la ufundi litaendelea kutuandaa na kutujenga kwa mchezo huo, tusubiri siku ifike," alisema.

Morrison ni kama ameamsha hisia za mashabiki wa Yanga kuelekea kwenye mchezo huo wa Jumapili kutokana na bao alilofunga dhidi ya Kagera.

Kabla ya mchezo huo kulikuwa na sintofahamu kwa mashabiki kujua mustakabali wa kiungo huyo kuelekea kwenye mchezo wao huo.

Ni wazi sasa uwepo wake kwenye mchezo huo utawapa shauku kubwa mashabiki wa Yanga kuelekea kwenye mchezo huo.

Mshindi wa mchezo huo atatinga hatua ya fainali na kuchuana na mshindi baina ya Sahare ya Tanga na Namungo ya Lindi watakaocheza nusu fainali nyingine.

Habari Kubwa