Msuva afurahia ndoto zimetimia

09Jan 2020
Somoe Ng'itu
Dar es Salaam
Nipashe
Msuva afurahia ndoto zimetimia

MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Simon Msuva, amesema ndoto zake za kucheza soka la kulipwa Ulaya zimetimia baada ya kukamilika kwa 'dili' la kujiunga na klabu ya Benfica ya Ureno.

MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Simon Msuva, picha mtandao

Msuva amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea timu hiyo lakini atapelekwa kwa mkopo wa miezi sita katika timu ya Pananthiakos.

Akizungumza na Nipashe jana, Msuva, alisema kuwa juhudi na bidii zake ndio zimefanikisha usajili huo na anaamini ataendelea kucheza soka la ushindani na kiwango cha juu ili kujiongezea thamani yake.

Msuva alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kufika hatua hiyo, kwa sababu hakuna kinachowezekana bila ya kuwapo na mipango mizuri.

"Nina furaha sana, ndoto zangu za kucheza Ulaya, kusajiliwa na klabu kubwa zimetimia," alisema kwa kifupi mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga.

Meneja wa mchezaji huyo, Dkt. Jonas Tiboroha, alisema kuwa Msuva anatarajiwa kutua Ureno ifikapo Januari 15, mwaka huu.

Yanga ilimuuza Msuva kwa Difaa El Jadida ya Morocco kwa dau la Dola za Marekani 100,000 mwaka 2016, lakini klabu hiyo ilikataa kuweka kipengele cha kulipwa fedha endapo atauzwa kwa timu nyingine.

Habari Kubwa