Msuva ampiku Kichuya Oktoba

06Nov 2016
Faustine Feliciane
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Msuva ampiku Kichuya Oktoba

WINGA wa Klabu ya Yanga, Simon Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Oktoba.

Simon-Msuva.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, ilisema katika tuzo hiyo Msuva alikuwa akishindana na wachezaji wawili wa Simba, Shiza Kichuya na Mzamilu Yassin.

"Kwa mwezi huo wa Oktoba kulikuwa na mizunguko sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist)," alisema Lucas.

Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu wa 2014/2015, atazawadiwa Sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo Kampuni ya Vodacom Tanzania.

Habari Kubwa