Msuva: Msinichukie, ndiyo soka

09Mar 2016
Bakari Kagoma
Dar
Lete Raha
Msuva: Msinichukie, ndiyo soka

WINGA wa Yanga, Simon Msuva amewataka wapenzi na mashabiki wa timu yake kuacha kumsema anapopoteza nafasi za kufunga kwani hiyo ndiyo soka.

Simon Msuva akijaribu kufunga goli.

Mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, amesema kwamba katika maisha ya soka kuna kupanda na kushuka, jambo ambalo mashabiki wa timu hiyo wanapaswa kuliheshimu.

Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya kukosa nafasi nyingi katika mchezo dhidi ya Azam, huku baadhi ya mashabiki wakisema yeye ndiye aliyepelekea timu yake kupata sare ya magoli 2-2 na kuwashusha hadi kushika nafasi ya pili baada ya klabu ya Simba kushinda dhidi ya Mbeya City.

“Inatokea katika mpira na sio kwangu tu, wachezaji wengi unakuta tena hata Ulaya, ila hapa kwetu ikitokea watu wanahamaki sana” alisema Msuva.

Katika mchezo huo, winga huyo alipiga krosi nne nzuri huku nane zikiwa ni fyongo kitu kilichosababisha mashabiki wa Yanga kuanza kumzomea, hadi kocha Mholanzi Hans van der Pluijm akamtoa kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Godfrey Mwashiuya.

Kabla ya hapo, katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius, kocha Pluijm alisema kama Msuva angetimiza majukumu yake ya uwanjani wangeweza kiubuka na ushindi mkubwa wa zaidi ya magoli sita.

Habari Kubwa