iliyobaki.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema kuwa, awali kulikuwa na makubaliano ya kiungo huyo anayemaliza mkataba wa miaka miwili kwenye klabu hiyo kwenda TP Mazembe kwa mkopo wa miezi sita, lakini yeye anaonekana mawazo yake bado anataka kubaki nchini.
"Makubaliano yetu ilikuwa ni kwamba aende TP Mazembe kwa mkopo. Tumempa nafasi hiyo, lakini mwenyewe anaonekana hana furaha ya kuondoka, yeye anataka kubaki Yanga, mpaka juzi ilikuwa hivyo, sisi kwenye mfumo wa usajili tulisharuhusu, lakini naona mwenyewe anaona abaki tu Tanzania, kwa hiyo tunaendelea kusubiri, tupate taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu kabla ya kutoa maamuzi," alisema Bumbuli.
Hata hivyo, alisema kama Tonombe akikataa haina shida kwa sababu klabu hiyo bado kikanuni ina pungufu ya mchezaji mmoja wa kigeni, hivyo haitaathiri usajili wa Chico.
Ofisa habari huyo pia amepinga kile kinachosemwa na baadhi ya watu kuwa usajili huo ni wa mabadilishano wa wachezaji na TP Mazembe, badala yake kuwa ni usajili wa kawaida tu.
"Hatutabadilishana, ila wao walikuwa na mahitaji ya kiungo, wakataka huduma ya Mukoko na sisi tulihitaji straika baada ya kuumia kwa Yacouba Songne," alisema.