Mwadui yaitisha kiaina Azam FC

07Feb 2016
Faustine Feliciane
Nipashe Jumapili
Mwadui yaitisha kiaina Azam FC

KOCHA wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwhelu 'Julio', amesema kuwa ataishangaza Azam FC kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa kuondoka na pointi katika mchezo wao leo hii.

Mchezo huo utakuwa kama alama ya kisasi cha mchezo wa kwanza mjini Shinyanga, Septemba 20 mwaka jana, ambapo Azam ilishinda bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji John Bocco.
Julio alisema anafahamu ugumu wa mchezo huo kwenye uwanja wa Azam Compelx, lakini wamejiandaa kuwashangaza wenyeji.
"Tutacheza mchezo huo kwa umakini mkubwa, tutashambulia na kukaba kwa wakati mmoja. Tumejipanga kwa ushindi," alisema Julio.
Alisema Azam wataingia uwanjani wakitaka ushindi hasa kutokana na hali ilivyo kwenye msimamo wa ligi.
"Wasitarajie mteremko kwetu, tunataka ushindi kwa sababu na sisi tunahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zetu."
Kikosi cha Mwadui kipo katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 28 baada ya mech 17.

Habari Kubwa