Mwambusi aitabiria makubwa Azam FC

14Jun 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mwambusi aitabiria makubwa Azam FC

KOCHA Juma Mwambusi, amesema Azam FC ina nafasi ya kufanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

KOCHA Juma Mwambusi.

Mwambusi ametua Azam kama kocha msaidizi na kuungana na Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm, ambaye naye amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni akitokea Singida United.

Wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja kwenye kikosi cha Yanga msimu wa 2015/16 na 2016/2017 kabla ya kila mmoja kuachana na timu hiyo.

Mwambusi, amesema amefurahi kujiunga na Azam kama kocha msaidizi akimsaidia Pluijm.

"Naamini baada ya muda Azam itakuwa tishio tena, natarajia kuliona hilo kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu," alisema Mwambusi.

Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuwa kocha msaidizi wa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati wa michuano ya Cecafa.

Azam imemchukua Pluijm na Mwambusi baada ya klabu hiyo kuachana na aliyekuwa kocha wake Aristica Cioaba raia wa Romania.

Habari Kubwa