Namungo sasa mguu mmoja makundi CAF

22Feb 2021
Adam Fungamwango
Dar es Salaam
Nipashe
Namungo sasa mguu mmoja makundi CAF

Namungo, wamejiwekea mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo, baada ya jana kuichakaza Club Despotrivo Primeiro de Agosto ya Angola kwa mabao 6-2 kwenye mechi iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Namungo FC, Stephen Sey, akichambua safu ya ulinzi ya CD de Agosto ya Angola kwenye mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam jana na Namungo kushinda 6-2. PICHA: JUMANNE JUMA

Ni mechi ambayo De Agosto ilikuwa mwenyeji kutokana Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuamuru ichezwe hapa Tanzania badala ya Angola, kutokana na sintofahamu iliyotoka nchini humo kwa kikosi cha Namungo kuzuiliwa Uwanja wa Ndege baada ya kutua Angola.

De Agosto ilianza kupata bao la kuongoza dakika ya 14 kupitia kwa mchezaji wake, Brian Moya. Hata hivyo ilikuwa ni uzembe wa mabeki wa Namungo, kwani kipa Joachim Naminana aliokoa, lakini mabeki bado walizubaa na mfungaji akaupiga tena kwa mara ya tatu na kuujaza wavuni. Alikuwa ni Hashim Manyanya alipoisawazishia Namungo dakika ya 32.

Baada ya bao hilo Namungo walicharuka na kufanikiwa kuogeza bao lingine dakika sita baadaye, lililowekwa ndani ya wavu na Sixtus Sabilo, akimalizia mpira uliotemwa na kipa Adao Cabaca, kufuatia shuti la Ralients Lusajo. Dakika ya 50, Waangola walipata bao la pili lililofungwa na Ambrosini Salvador.

Lusajo aliipatia Namungo bao la tatu kwenye dakika ya 55, Sabilo akifunga la nne dakika ya 59. Kuingia kwa Idd Kipagwile kuliisaidia Namungo kwani, kona zake mbili zilizaa mabao yaliyofungwa na Erick Kwizera, huku Steven Sey akifunga bao la sita. Dakika ya 82, Nahimana aliokoa penati nyingine iliyopigwa na Moya na kuiweka salama Namungo. Timu hizo zitarudiana kwenye uwanja huo Alhamisi wiki hii na endapo Namungo itapata matokeo ya jumla itatinga hatua ya makundi.

Habari Kubwa