Nape akumbuka nyasi bandia Nyamagana

29Mar 2016
Daniel Mkate
Mwanza
Nipashe
Nape akumbuka nyasi bandia Nyamagana

WAZIRI Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema atahakikisha Uwanja wa Nyamagana uliosimama kwa muda mrefu kuwekwa nyasi bandia, unaanza kushughulikiwa.

waziri, Nape Nnauye.

Nnauye alitoa ahadi hiyo juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika jijini Mwanza na kuhudhuriwa na waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya nchi.

“Nimekumbushwa kuhusu nyasi bandia na Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, nawahakikishia naanza kushughulikia kuanzia sasa ili uwanja huo uanze kutengenenzwa,” alisema Nnauye.

Alisema atakutana na Mabula ili kufahamu tatizo lililopo kabla ya kuanza kushughulikia.

Uwanja wa Nyamagana ulisimama kufanyika kwa shughuli zote za michezo baada ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), kuuweka katika mpango wa kuweza nyasi bandia, lakini licha ya shughuli hiyo kuanza, ghafla ilisimama kutokana na serikali kutaka nyasi zilizopo bandarini kulipiwa ushuru.

Habari Kubwa