Ndanda Kosovo afariki dunia

10Apr 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe Jumapili
Ndanda Kosovo afariki dunia

MWANAMUZIKI Ndanda Kosovo (44), amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

kosovo

MWANAMUZIKI Ndanda Kosovo (44), amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Ndanda aliyekuwa maarufu kwa jina la 'Kichaa' au 'Mjelajela" alipata umaarufu akiwa na bendi ya FM Academia baada ya wanamuziki wake kuswekwa lupango kutokana na kukosa kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja wa bendi ya FM Academia, Kelvin Mkinga Ndanda alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu.

Mkinga alisema kuwa taratibu za mazishi za mwanamuziki huyo wa zamani wa FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' zitatolewa kati ya leo na kesho baada ya familia ya marehemu huyo kukutana na kufanya uamuzi. Marehemu aliondoka FM Academia na kwenda kuanzisha bendi ya Stono Musica.

Habari Kubwa