Ndayiragije amgusa Kaseja kurudi Stars

25Mar 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Ndayiragije amgusa Kaseja kurudi Stars

WAKATI Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Etienne Ndayiragije, akisema atalazimika kuita wachezaji wapya wa kuunda kikosi chake mara ratiba mpya ya michuano ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2021 na Fainali ya Wachezaji wa Ndani (CHAN), kipa .....

Kipa wa KMC, Juma Kaseja, ambaye alifanya kazi kubwa ya kuiwezesha Taifa Stars kufuzu Fainali za CHAN zilizotarajiwa kuanza Aprili 4-25, mwaka huu nchini Cameroon kabla ya kuahirishwa. Mlindamlango huyo amepania kurejea katika kikosi cha Stars baada ya awali kuachwa kutokana na kuwa majeruhi. PICHA: MAKTABA

mkongwe nchini, Juma Kaseja amepania kuwamo ndani.

Taifa Stars ilivunja kambi yake ya kujiandaa na mechi ya kufuzu Afcon na dhidi ya Tunisia pia kujiwinda na michuano ya CHAN, baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuahirisha mchezo na michuano hiyo kutokana na kasi ya kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19) duniani.

Na Tayari Ndayiragije amesema atalazimika kuita kikosi chake upya kulingana na kiwango watakachoonyesha wachezaji wakati ukifika, jambo ambalo Kaseja amepania kurejea baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti.

Kaseja alimwambia mwandishi wetu kuwa atapambana kurejesha kiwango chake baada ya kupona maumivu ya goti ili awe fiti na kurejeshwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya fainali za CHAN.

“Nitapambana, nitarejesha kiwango, na ninaamini nitakuwamo kwenye timu,” alisema Kaseja ambaye ni kipa wa klabu ya KMC, baada ya kuzitumiakia pia Moro United, Simba, Yanga, Mbeya City na Kagera Sugar.

Habari Kubwa