Ndugai aipongeza Simba kuwa bingwa,Yanga kukaa kileleni muda mrefu

22May 2019
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Ndugai aipongeza Simba kuwa bingwa,Yanga kukaa kileleni muda mrefu

Spika wa Bunge Job Ndugai ameipongeza timu ya Simba kwa kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019-2020 lakini pia ameipongeza timu ya Yanga kwa kufanya juhudi ya kuongoza Ligi kwa muda mrefu.

"Tuwapongeze sana Simba kwa kunyakua ubingwa 2019-2020,Hongereni sana Simba lakini pia niwapongeze sana watani wetu Yanga kwa kufanya juhudi ya kuongoza Ligi kwa muda mrefu,"-Spika Job Ndugai

Hata hivyo akizungumza mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni leo, Ndugai amesema Bunge Sports Club wanaendelea kuratibu utaratibu wa Wabunge kwenda nchini Misri kushuhudia fainali za michuano ya Mataifa Afrika(AFCON).

Amesema safari hiyo ya Misri itaongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na yeye Spika Ndugai.

Ndugai amewataka Wabunge kuendelea kujiorodhesha kwa ajili ya kwenda kuishangilia timu ya Tanzania kwenye michuano hiyo.

“Masuala ya nauli ni vema Wabunge tuonesha mfano tukajiandikisha wengi na kuwahamasisha wengine inabidi mpango iende haraka kwa sababu Booking za hoteli zitajaa itabidi tufanye mapema, Tujiandikishe mapema naamini itawapa moyo vijana wetu,”amesema Spika Ndugai.

 

Habari Kubwa