Ne-Yo kutumbuiza Mwanza Mei 21

09May 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Ne-Yo kutumbuiza Mwanza Mei 21

Mwanamuziki wa Marekani, Ne-Yo anatarajia kufanya ziara ya muziki nchini baadaye mwezi huu kwa mwaliko wa Kampuni ya Vodacom.

Ne-Yo

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Vodacom, Matina Nkurlu mwanamuziki huyo wa kizazi kipya atatua nchini Mei 19 na siku mbili baadaye atatumbuiza kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza katika tamasha la lililoandaliwa na kampuni hiyo 'Jembeka na Vodacom'.

Nkurlu alisema Vodacom inatambua umuhimu wa sanaa ya muziki nchini, hivyo wameamua kumleta msanii huyo ili kuwapa Watanzania vionjo vya muziki wa kimataifa.

Ne-Yo anatamba na vibao kama Let Me Love You, Beautiful Monster, Coming With You na She Knows Featuring.
Mbali na kutoa burudani ya muziki, pia msanii huyo atashiriki katika shughuli za kusaidia jamii kupitia taasisi ya Vodacom Foundation.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa Tamasha la Jembeka, Costantine Magavilla, alisema anaamini msanii huyo atateka nyoyo za wapenzi wa muziki katika jiji hilo kutokana na uwezo wake wa kutawala jukwaa.

Habari Kubwa