Neymar akosolewa kutangaza kustaafu

14Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Neymar akosolewa kutangaza kustaafu

KAULI ya Neymar kwamba, Kombe la Dunia 2022 linaweza kuwa ndiyo mwisho wake wa kuichezea Timu ya Taifa ya Brazil imekosolewa na nyota wa zamani wa Paris Saint-Germain, Jerome Rothem.

“Ujumbe wake wa hivi karibuni ni wa kutisha kwa PSG,” alisema Rothen.

“Amekosa kujitolea kwenye klabu anafanya siyo sawa. Neymar ni mchezaji mzuri sana akiwa katika ubora wake, lakini tatizo ni kwamba anakosa ujasiri.

“Upendo alionao kwa Brazil ni dhahiri najua kwamba, anataka kushinda Kombe la Dunia.

“Nafasi yake ya mwisho itakuwa nchini Qatar mwaka ujao, lakini nadhani anapaswa kukabiliana na majukumu yake.”

Neymar mwenye umri wa miaka 29 aliiambia DAZN, “Nadhani mwaka 2022 nchini Qatar itakuwa michuano yangu ya mwisho, kwa sababu sijui kama nitakuwa sawa kiakili na kimwili kukabiliana na soka tena.