Ngoma atamba makali yamerejea

12Jan 2019
Na Mwandishi Wetu
Zanzibar
Nipashe
Ngoma atamba makali yamerejea

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Donald Ngoma amesema kuwa ubora wake umerejea na sasa atakuwa anafunga mabao katika kila mechi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ngoma alisema anapofanikiwa kufunga bao hayo ni matunda ya kutumia vizuri nafasi anazopata na kwake hilo ni jambo la kawaida kwa sababu ndiyo kazi yake.

Ngoma alisema ili mchezaji uweze kufanya vizuri zaidi hususani katika ufungaji wa magoli inapaswa kusikiliza vyema maelekezo kutoka kwa kocha wako na ukifanya hivyo utakuwa na mafanikio uwanjani.

"Mimi huwa ninasikiliza zaidi kocha anataka nini, hali inayomfanya aweze kumalizia vizuri pindi anapoelekea golini kupachika bao.Ukisikiliza vizuri maelekezo ya kocha, ukiyafanyia kazi basi unakuwa mfungaji mzuri zaidi na hata umaliziaji wako pia unakuwa mzuri, hii ndio imenifanya mimi nione kitu cha kawaida kufunga goli," alisema Ngoma.

Aliongeza kuwa mchezaji kupangwa katika kikosi cha kwanza cha timu haimaanishi nyie ndio bora zaidi au ni wazuri bali ni uamuzi na mipango ya benchi la ufundi.