Ngoma: Mechi tano zitatupa sura ya ubingwa

09Mar 2016
Lasteck Alfred
Dar
Lete Raha
Ngoma: Mechi tano zitatupa sura ya ubingwa

MBALI na kudai kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara ni ligi ngumu kuliko ile ya kwao Zimbabwe, Straika wa Yanga, Donald Ngoma amedai kuwa ametazama jinsi ubingwa unavyowania na kasha akasema,

Donald Ngoma.

“ Tunahitaji kushinda mechi tano zijazo tena kwa mabao mengi kabla ya kumalizia nyingine ambazo zitakuwa na ugumu wa kipekee.

Ngoma aliyetokea Platinum FC ya Zimbabwe alisema,” Kuna ushindani mkubwa kipindi hiki ambacho mechi zimebaki kidogo ili ligi imalizike.

“Inatubidi tupambane kuhakikisha tunashinda mechi tano zijazo kwa idadi isiyopungua mabao matatu ili inapotokea suala la kupewa ubingwa kwa tofauti ya mabao basi tunakuwa na mabao mengi kuliko timu yoyote.

“Pia nimesema tunahitaji kuweka mkazo kwenye mechi hizi tano kwa kuwa ni mechi ambazo zinaweza kutupeleka pazuri. Mechi tano za mwisho huwa ni ngumu kwa kuwa kila timu huwa inapigana kufa kupona kujiweka kwenye nafasi fulani.

“Timu zilizopo chini kwenye msimamo huwa zinapambana kupanda ili kujinusuru hivyo huwa zinafanya mechi kuwa ngumu na kama ni kupata ushindi basi unaweza kuambulia idadi ndogo ya mabao,”alisema Ngoma ambaye mpaka sasa amefunga mabao 12.

Mbali na African Sport wanayocheza nayo leo kwenye uwanja wa Taifa, mechi nyingine nne ambazo Ngoma anazitazama kuwa zitatoa mwelekeo wa jinsi Yanga itakavyotwaa ubingwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Toto African, Mwadui na Kagera Sugar.

Kisha watabiki na michezo mitano kabla ya Ligi kuisha.Mechi hizo ni dhidi ya Stand United, Mgambo JKT, Mbeya City, Ndanda na Majimaji.

Habari Kubwa