Ngorongoro Marathon kufanyika Agosti

11Jul 2020
Shufaa Lyimo
Arusha
Nipashe
Ngorongoro Marathon kufanyika Agosti

WANARIADHA kutoka sehemu mbalimbali nchini watachuana katika mbio za Ngorongoro Marathon ambazo zimepangwa kufanyika Agosti 2, mwaka huu kwenye Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, imefahamika.

Akizungumza na gazeti hili jana, mwanariadha maarufu nchini, Alphonce Simbu, alisema anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya kushiriki mbio hizo.

Simbu alisema anaamini mashindano hayo yataanza kurejesha viwango vya wanariadha ambao walikaa muda mrefu bila ya kushiriki michuano kutokana na janga la corona.

"Kwa upande wangu naendelea na mazoezi ili kuuweka mwili wangu sawa kuelekea mbio hizo, ninajituma sana kwa sababu nilikaa muda mrefu bila kushiriki mashindano yoyote," alisema Simbu.

Mwanariadha huyo alimewaomba Watanzania waendelee kuyaombea mataifa mengine ambayo bado wanachangamoto kubwa ya ugonjwa wa COVID 19 ili virusi vya ugonjwa huo vimalizike na maisha yao yaendelee kama zamani ikiwamo michezo.

"Tushirikiane kwa umoja wetu kuziombea nchi zote ambazo zinasumbuliwa na ugonjwa huo, tunahitaji kuona maisha mengine yaendelea, tuondokane na janga hili," alisema Simbu.

Habari Kubwa