'Nitaifuta machozi Tanzania Olimpiki'

16Mar 2016
Dar
Nipashe
'Nitaifuta machozi Tanzania Olimpiki'

BAADA ya kupata medali ya shaba katika mashindano ya Lake Diwa Marathon yaliyofanyika Japan hivi karibuni, mwanariadha Alphonce Felix ametamba kuwa mwaka huu Tanzania haitakwenda 'kutalii' kwenye Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Agosti jijini Rio de Janeiro, Brazil.

mwanariadha Alphonce Felix.

Felix ambaye amefuzu kushiriki katika mashindano hayo, anaendelea na mazoezi kwenye kambi ya timu ya taifa ya riadha iliyoko mkoani Kilimanjaro chini ya kocha mkuu, Francis John.

Akizungumza na gazeti hili jana, Felix alisema yeye na wanariadha wengine walioko kambini Moshi, wanajituma kuhakikisha viwango vyao vinapanda na hatimaye kwenda kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania kwenye michezo hiyo mikubwa.

"Safari hii nimejipanga vizuri kuhakikisha naibeba nchi yangu katika Michezo ya Olimpiki, ninakwenda kushindana si kushiriki, tunataka kufanya maajabu," alisema Felix.

Naye kocha wa timu hiyo (John) alisema wanariadha wake wanaendelea vizuri na mazoezi na kueleza kila siku wanafanya mazoezi asubuhi na jioni na akiwakimbiza umbali mrefu.

Habari Kubwa