Nonga: Juhudi binafsi zilitubeba

03Apr 2016
Lete Raha
Nonga: Juhudi binafsi zilitubeba

MSHAMBULIAJI wa Yanga Paul Nonga amesema juhudi binafsi za wachezaji wa Yanga zimechangia kwa kiasi kikubwa kutoka na ushindi katika mchezo dhidi ya Ndanda FC.

Paul Nonga, akimlamba chenga beki wa Friends Rangers.

Nonga alisema Ndanda walikuja kwa lengo la kuhakikisha wanaifunga Yanga, lakini walijikuta wakitoka vichwa chini kutokana na kupoteza nafasi.

Akizungumza na gazeti hili mara baada ya mchezo huo, alisema ilikuwa mchezo mgumu lakini tulijipanga uwanjani kuhakikisha tunawavuta na kupata bao la ushindi.

Alisema pamoja na rafu ambazo zimechezwa uwanjani dhidi yao, lakini walipambana kuhakikisha ushindi unapatikana.
Alisema kwa matokeo hayo, kikosi chao kinaendelea na mazoezi chini ya kocha wao Hans Van Pluijm kuhakikisha timu yao inafanya vizuri katika mashindano hayo.

Habari Kubwa