Nsajigwa awapa somo Yanga kuhusu APR

06Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Nsajigwa awapa somo Yanga kuhusu APR

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa na klabu ya Yanga Shadrack Nsajigwa aliitaka timu yake hiyo kuwa makini sana katika wa klabu bingwa dhidi ya APR ya Rwanda.

Kikosi cha wachezaji wa APR

Nsajigwa alitoa rai hiyo baada ya kuona mwenendo mzima wa timu yake kutokana na kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika mechi zake na hivyo kusema kuwa itawagharimu kama mtindo huo utaendelea kwenye mechi dhidi ya APR.

“Ni mechi ambayo itakuwa kipimo kizuri kwa Yanga kutokana na ubora wa timu zote mbili, ila uzembe wowote utaofanya na timu utaigharimu” alisema Nsajigwa.

Beki huyo wa zamani wa kulia hakusita kuimwagia sifa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inayoongozwa na Amisi Tambwe na Donald Ngoma na kusema ni miongoni mwa safu tishio za upachikaji mabao nchini.

“Tambwe na Ngoma wametengeneza uelewano mzuri uwanjani ambao umesaidia kupatikana kwa magoli mengi msimu huu” alisema Nsajigwa.

Katika mchezo huo utakao fanyika Mei 12 nchini Rwanda utawarejesha nyumbani wachezaji waliowahi kuitumikia timu hiyo Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite.

Habari Kubwa