Nyoni hakusafiri pamoja na wachezaji wenzake kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia, lakini jana mchana aliwasili Cameroon na kujiunga na kikosi hicho tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Limbe/Buea majira saa moja usiku.
Akizungumza na Nipashe kutoka Cameroon jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Cliford Ndimbo, alisema tayari Nyoni amewasili Cameroon na kujiunga katika kambi ya Stars.
"Amewasili leo mchana (jana) na moja kwa moja amejiunga na wenzake tayari kwa maandalizi ya michuano inayotukabili, ambapo keshokutwa (kesho) tutacheza dhidi ya Zambia," alisema.
Kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Ndimbo alisema yanaendelea vizuri na morali ya wachezaji iko juu kwa timu nzima...soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com