Nyota wa majaribio Simba washindwa kutoboa

13Jan 2021
Adam Fungamwango
Dar es Salaam
Nipashe
Nyota wa majaribio Simba washindwa kutoboa

WACHEZAJI wapya walioletwa klabu ya Simba kufanya majaribio, ni kama tayari wameshindwa baada ya kushindwa kuonyesha ubora wao kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, imeelezwa.

Wachezaji hao ni Benard Agele 'Coulibaly' kutoka Sudan Kusini, Kelvin Moyo na Ian Nyoni wote kutoka Zimbabwe, ambao wameshindwa kuwaridhisha mabosi wa klabu hiyo, benchi la ufundi na hata wanachama na mashabiki wa timu hiyo.

Habari za ndani kutoka Zanzibar zinaeleza wachezaji hao ambao walishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayomalizika leo kwenye fainali kati ya Simba na Yanga, wameonekana kutokidhi matakwa ya benchi la ufundi.

"Imeonekana kuwa viwango vyao ni vya kawaida sana, ni kama vya wachezaji tulionao tu kwenye klabu ya Simba na hata hapa Tanzania, kwa hiyo sidhani kama kuna hata mmoja atakayesajiliwa," kilieleza chanzo chetu.

Lakini Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Selemani Matola, aliwatetea akieleza wachezaji huko walikotoka ligi zao zimesimama kwa hiyo hawana utimamu wa mwili.

"Unajua wengi wa wachezaji wanaokuja kwa majaribio ligi zao kwenye nchi wanazotoka zimesimama kwa hiyo hawako fiti, hawana utimamu wa mwili kwa sasa. Hata mechi nilizowapa walikuwa wanalalamika misuli na mpaka sasa hawako vizuri sana, nikaona bora niwapumzishe kwenye mechi ya Namungo na kuwatumia zaidi wachezaji ambao wako tayari kucheza mashindano hayo.

Hata hivyo, Matola hakusema kama watasajiliwa au wataachwa, lakini taarifa zinadai kuwa wameonekana hawatoshi kuichezea klabu kama Simba inayotaka wachezaji ambao wako tayari kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika....soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa