Omog: Kwa mfano Prisons itatokaje?

09Nov 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Omog: Kwa mfano Prisons itatokaje?

KOCHA wa Simba, Mcameroon Joseph Omog, amesema machungu ya timu yake kupoteza mchezo uliopita watayamaliza leo kwa kuondoka na pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons kwa kuwa timu hiyo haitakuwa na pakutokea.

Simba kwa mara ya kwanza msimu huu, Jumapili iliyopita walipoteza mchezo wao wa kwanza kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru.

Lakini Omog jana aliliambia Nipashe kuwa watacheza kwa tahadhari huku wakiwa na dhamira ya ushindi ili kurejea kwenye mstari wao wa ushindi kwa kila mechi.

"Naamini yaliyotokea Jumapili hayawezi kujirudia, makosa madogo madogo yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita tayari nimeyafanyia kazi," alisema Omog.

Hata hivyo kwa upande wa kocha wa Tanzania Prisons, Abdul Mingange, alisema wapinzani wao wasitegemee mtelemko kwenye mchezo wa leo.

Mchezo mwingine wa kiporo leo utashuhudia Azam iliyokutana na kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Mbao FC ya jijini Mwanza, ikiumana na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

Habari Kubwa