Origi atua rasmi Milan

29Jun 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Origi atua rasmi Milan

DIVOCK Origi amepigwa picha akiwa jijini Milan akijiandaa kukamilisha uhamisho wa kujiunga na wababe hao wa Italia kutoka Liverpool.

Mkataba wa mshambuliaji huyo unaisha mwishoni mwa mwezi huu na anatazamiwa kujiunga na Rossoneri hao kwa uhamisho wa bure.

Kama ilivyoripotiwa na 90min, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alifikia makubaliano ya maslahi binafsi na washindi hao wa Serie A, Mei mwaka huu, akikataa ofa kutoka kwa klabu kadhaa za Ligi Kuu England.

Zaidi ya mwezi mmoja baadaye, Origi sasa amesafiri hadi Milan kukamilisha uhamisho wake.

Mwandishi wa habari wa Italia, Daniele Longo alishiriki video ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akitoka kwenye uwanja wa ndege wa jiji hilo na kupiga picha Jumatatu jioni.

Origi alikuwa amepewa ofa mpya na Liverpool lakini akakataa huku akitafuta soka la kucheza kikosi cha kwanza.

Mbelgiji huyo mara nyingi amekuwa sio mchezaji chaguo la kwanza kwa kocha, Jurgen Klopp, akianza chini ya michezo 40 katika muda wake pale Anfield.

Habari Kubwa