Pamoja na kipigo, Twiga Stars wapozwa

09Mar 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Pamoja na kipigo, Twiga Stars wapozwa

LICHA ya kupoteza mechi dhidi ya Zimbabwe, wachezajj wa timu ya soka yaTaifa ya wanawake, Twiga Stars, jana wamepewa motisha na kutakiwa kuwaondoa wapinzani wao hao katika mechi ya marudiano.

Twiga stars

Twiga Stars ililala mabao 2-1 katika mechi iliyofanyika Ijumaa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Chamazi kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura aliwakabidhi wachezaji wa Twiga Stars Sh. 300,000 kila mmoja kama alivyoahidi kabla ya mechi hiyo.

Naibu Waziri huyo alisema amewapa wachezaji hao fedha hizo ili kusheherekea vizuri siku ya wanawake na kuwasisitiza kupambana ugenini na kushinda.

Twiga Stars inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo wa marudiano utakaofanyika Machi 20 na mshindi wa jumla akitarajiwa kukutana na Zambia au Namibia.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma alishukuru kwa niaba ya wachezaji na kwamba motisha hiyo ni deni la wao kwenda kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano.

Habari Kubwa